September 24, 2013

MFAHAMU REDDS MISS TANZANIA 2013,HAPPINESS WATIMANYA
 Happy (19) ni mzaliwa wa familia ya kawaida sana ya Mr Louis Roussos ya Morogoro. Wadogo zake Angel na Romeo sasa wanasoma St. Constantine shule iliyomtoa Happy. Pia, Happiness Watimanywa amewahi kusoma Laureatte International School ya Dar-es-salaam, ambapo akiwa hapo, alikutana na mwalimu wa michezo Mr Tchalewa Ndeki ambaye alimfungulia mipaka mingi Happy. Akiwa Laureatte, Happy aliwahi kwenda China na South Korea akiwa na wanafunzi wenzake katika matamasha mbali mbali ya elimu na michezo. Baada ya kumaliza kidato cha nne, Happy alifanikiwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Strathclyde cha UK ambapo anasomea digrii ya Biashara.

 Happiness Watimanywa, msichana pekee kutoka Tanzania aliyeweka historia ya kuongoza nchi zaidi ya 150 za mtandao wa IGCSE katika somo la Uhasibu kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka 2010.
 Kipindi ambacho Happy yupo kwenye likizo ndefu, alipata wakati mgumu wa kutokuwa na kitu cha kufanya, hivyo Happy aliamua kujihusisha na masuala ya urembo na kufanikiwa kutwaa Taji la Miss Dodoma, na Miss Kanda ya Kati na hatimaye kuingia kwenye kambi ya Miss Tanzania.
HAPPINESS AKIWA NA RIO PAUL
Ndani ya kambi ya Miss Tanzania, Happiness Watimanywa amekuwa mwiba kwa warembo wengine 29 wanaowania taji hilo kwani amekuwa akionesha uwezo wa hali ya juu kuanzia kwenye kipaji hata michezo, ukiachilia mbali upeo mkubwa alio nao.Hatimaye usiku wa tarehe 21 Happiness alifanikiwa kulitwaa Taji la Redds Miss Tanzania 2013